International Development Research Centre (IDRC) Canada     
idrc.ca HOME > IDRC Publications > IDRC Dossiers > TEHIP > Lessons >
 Topic Explorer  
TEHIP
     Issue
     Research
    Lessons
        Slide show
        TEHIP Briefs

IDRC in the world
Subscribe
Development Dossiers
Free Online Books
IDRC Explore Magazine
Research Programs
 People
Bill Carman

ID: 68378
Added: 2004-12-15 10:09
Modified: 2004-12-15 10:19
Refreshed: 2006-01-25 16:03

Click here to get the URL for the RSS format file RSS format file

FIXING HEALTH SYSTEMS / Swahili Executive Summary
Prev Document(s) 7 of 9 Next

UIMARISHAJI WA MIFUMO YA AFYA

 

 

UTANGULIZI

 

Nchi za Bara la Afrika hususan Kusini mwa Jangwa la Sahara zimekabiliwa na matatizo mengi ya afya. Matatizo ambayo yamelikumba bara hili ni pamoja na malaria, ukimwi, kifua kikuu, utapia mlo na ukosefu wa damu.Ukubwa wa tatizo hili umechangiwa zaidi na ukosefu wa nyenzo na umaskini. Hata hivyo hivi karibuni jamii ya kimataifa imeanzisha mfuko kukabiliana na tatizo hili.

 

Lakini mfuko huu pekee utaweza kuleta mafanikio yanayotarajiwa? Mradi wa Uimarishaji wa Huduma Muhimu za Afya (MUHUMA) ulianzishwa mwaka 1997 katika wilaya mbili za Rufiji na Morogoro ili kuweza kuhakiki endapo matumizi ya  raslimali ndogo zilizopo yatalenga kwenye mikakati inayoweza kupunguza kwa wingi athari za magonjwa. Mradi huu uliimarisha utendaji wa timu za menejimenti za afya wilayani kwa kuzipatia nyenzo, mikakati na fedha ambazo ziliwezesha timu kulenga nguvu zao katika kutatua matatizo yaliyokuwa yanaleta athari kubwa za kijamii.

 

Ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na Shirika la Kimataifa la Maendeleo na Utafiti la Canada (IDRC) umewezesha MUHUMA kuzipatia timu za menejimenti ya afya katika wilaya hizo mbili  nyenzo, mikakati na fedha. Wilaya hizo zimeweza kutumia raslimali kidogo na kuweka mikakati kutokana na raslimali hiyo kwa kuweka malengo ambayo yameweza kuboresha mfumo wa utoaji wa huduma bora za afya.

 

Matokeo ni kwamba kumekuwa na kupungua  kwa vifo katika wilaya zote mbili hasa miongoni mwa watoto watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Kupungua huko kumeziweka wilaya za Rufiji na Morogoro kuweza kufikia malengo ya Milenia ya  Umoja wa Mataifa katika kupunguza vifo miongoni mwa watoto kwa theluthi mbili ifikapo mwaka 2015, na hivyo kuleta matumaini.

 

 

UTAFITI

 

Taarifa zilizokusanywa kupitia mfumo wa  takwimu za vizazi na vifo zilitumika kuanzisha mpango huu katika wilaya hizi mbili. MUHUMA iliandaa mfumo unaotumia  komputa ambao ni rahisi kuutumia ulioziwezesha wilaya kupanga bajeti zao. Mfumo huo unatoa kipaumbele kwa kutenga fedha kwenye huduma za afya zinazotatua  magonjwa ambayo yanajitokeza zaidi katika jamii yao.  Vifaa hivyo ambavyo vinaweza kutumika mahali pengine tayari vinaandaliwa kuweza kutumiwa katika wilaya nyingine hapa nchini.

 

Kwa kutumia  mfumo huu  timu za manejimenti ya afya katika ngazi ya wilaya zimeweza kurekebisha bajeti zao   ili kuweka mkazo zaidi katika matumizi kwa magonjwa yale ambayo yanasababisha vifo ikiwemo malaria, magonjwa ya watoto wadogo, chanjo n.k. Timu hizo zimegundua hata hivyo kwamba ili kuweza kukabiliana na hali hii ni  muhimu kuongeza nguvu kazi kuanzia  kliniki za vijijini mpaka kwenye mfumo mzima wa afya wilayani.

 

Hii ilizifanya timu za afya za wilaya kuongeza matumizi katika mafunzo ya  watumishi wa ugani,  kuhusu magonjwa ya watoto, mawasiliano, usimamizi , utoaji na usambazaji wa madawa.

 

Katika   kipindi kifupi mahudhurio ya wagonjwa kwenye vituo vya afya yaliongezeka. Katika wilaya zote mbili hali ya vifo imeshuka  miongoni mwa watoto na hata kwa watu wazima.

 

 

TULIYOJIFUNZA NA MAPENDEKEZO

 

Uzoefu katika wilaya HIZI mbili hapa Tanzania unaonyesha kuwa kuwekeza katika mifumo ya afya ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za afya na kulenga matatizo muhimu ya kiafya kunaweza kuleta manufaa. Jambo la msingi ambalo MUHUMA  imejifunza ni kwamba Taasisi za kimataifa na ngazi mbalimbali za serikali lazima zifikirie na kuipa kipaumbele mifumo ya afya pamoja na kuangalia tiba mpya, dawa na chanjo. Nyenzo na mikakati mingine ya utekelezaji pia vimeonyesha kuwa vya muhimu kwa timu za afya za wilaya zinazotaka kuboresha huduma hizo katika maeneo yao. MUHUMA  hivyo inatoa wito kwa nchi nyingine zinazoendelea kutumia nyenzo na mikakati hiyo kwani imeandaliwa kuweza pia kutumika katika nchi zingine.

 

Mambo mengine muhimu ni pamoja na;

 

Programu zinazowekeza katika mifumo ya afya ziangalie umuhimu wa kuunganisha masuala ya utafiti na maendeleo kwa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi. Mkakati huu utawezesha utafiti kufanyika haraka ili kuendeleza programu kwa kupitia mapendekezo yaliyotolewa na watafiti.

 

Kuwekeza katika nguvu kazi ni muhimu. Utoaji wa huduma bora za afya moja kwa moja unategemea watoaji huduma wa msingi na waliowezeshwa. Kuwekeza katika suala la mafunzo, elimu na kuandaa mtaala mpya ni muhimu.

 

Ipo pia haja ya kuwekeza vya kutosha katika miundo mbinu kwa mfano zahanati, usafiri na uimarishaji wa habari na mawasiliano.

 

Vipaumbele katika ufadhili  na utekelezaji lazima vilenge jamii katika hali halisi ya mazingira na mipango inayolenga kutatua magonjwa yaliyopo mahali pale badala ya kufuata matakwa ya wahisani.

 

Miradi ya afya ni vizuri uzoefu wake ukawa endelevu na kuweza kurekebishika sehemu zingine kwa kufuata mazingira.

 

Kuna haja kwa waangalizi wa masuala ya afya kuyaweka pamoja masuala yanayohusiana kati ya afya na umaskini katika hali ambayo itawafanya watoaji wa maamuzi waweze kuyaelewa barabara na kuchukua hatua. Mfumo wa kuwa na kanda (sentinel) za uchunguzi na utoaji habari toka kwenye kaya unaweza kutoa takwimu hizo ambazo ni muhimu kwa nchi mbali mbali ambazo hazina utaratibu wa kuweka kumbukumbu muhimu.

 

 

Mwisho







Prev Document(s) 7 of 9 Next



   guest (Read)(Ottawa)   Login Home|Jobs|Important Notice|General Infomation|Contact Us|Webmaster|Low Bandwidth
Copyright 1995 - 2005 © International Development Research Centre Canada     
Latin America Middle East And North Africa Sub-Saharan Africa Asia IDRC in the world